Matokeo 6 katika mwili wako kama ukila ndizi 2 kila siku.

Ndizi zina virutubisho vingi kama vile vitamini, nyuzinyuzi, protini, wanga, madini ya chuma na virutubisho vya sukari kama ‘Sucrose’ na ‘Fructose’. Wataalam wa lishe wanasema kula ndizi mbili kwa siku kwa muda wa mwezi tu, afya yako itaimalika.

Kuondokana na tatizo la Kiungulia
Ndizi kiasili sio tunda lenye asidi kwa wingi, ikumbukwe kuwa kiungulia husababishwa na uwepo wa asidi nyingi mwilini. Hivyo ndizi ni tiba kwa wote ambao wanasumbuliwa na kiungulia. Kula japo ndizi moja kwa siku basi itatuliza haraka na kuondoa dalili zote za kiungulia.

Kuondoa Presha
Ndizi pia zina wingi wa madini ya ‘Sodiam’ na ‘Potassium’ ambayo huweka sawa presha ya damu na kuimarisha afya ya moyo. Madini hayo pia husaidia kutanua misuli ya moyo ili kufanya kazi zake kwa urahisi.

Kuongeza Nguvu
Endapo utakula ndizi mbili kabla ya kazi yoyote hakika nguvu zako zitaongezeka. Kama ilivyoelezwa awali ndizi zina vitamini, madini, wanga, na ‘Glycemic’ (kiwango cha sukari yenye kutia nguvu mwilini) ambavyo vyote hivyo ni vyanzo vizuri vya kutia nguvu mwilini kwa haraka.

Kuondokana naugonjwa wa Vidonda vya tumbo
Ndizi zina mchanganyiko wa vilainishi na nyuzinyuzi ambazo hulainisha tumbo na kupelekea kuzuia mikwaruzo kwenye utumbo hivyo kuzuia vidonda vya tumbo.

Husaidia wagonjwa wa Anaemia
Anaemia kitaalamu ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini, madini hayo husaidia kwenye uzalishaji wa chembechembe za damu nyekukundu ambazo huhitajika kwa wingi mwilini.

Ndizi zina madini ya chuma ambayo huwasaidia wagonjwa wa Anaemia kwa sababu madini ya chuma husukuma uzalishaji wa ‘Haemoglobin’. Hivyo huongeza chembechembe nyekundu za damu na kuongeza mzunguko wa damu mwilini.

Haemoglobin ni protini inayopatikana kwenye chembechembe nyekundu za damu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kutoka kwenye mapafu na kwenda sehem mbalimbali za mwili, Aidha huchukua pia hewa ya Kabondayoksaidi kutoka kwenye viungo vya mwili na kurudisha kwenye mapafu.
Wakati mwengine ugonjwa wa Anaemia hujulikana kama Upungufu/Ukosefu wa damu mwilini.

Huondoa mgandamizo wa mawazo
Ndizi zina muunganiko wa pekee ambao kitaalam huitwa ‘Tryptophan’ hii ni asidi inayopatikana kwenye protini, ambayo husaidia kwa kutotokea mgandamizo wa mawazo. Virutubisho hivi vikiingia mwilini vinabadirika na kuwa ‘Serotonin’ ambayo hupatikana moja kwa moja kwenye ubongo, huweka misuli sawa na husaidia mtu ajisikie furaha na kuondokana na mawazo.
>

1 comment: