Harmorapa Nae Aamua Lazima Amuoe Wema Sepetu…Aanza Mikakati
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa ambaye hakauki kwenye mitandao kwa vitendo vyake vya kiki, amesema na amini naye ipo siku atatimiza ndoto zake na kumuoa Wema Sepetu kama alivyofanya Dogo Janja kwa Uwoya.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmorapa ameandika ujumbe akisema kwamba hatokuja kukata tamaa juu ya ndoto yake ya kumng’oa ‘Tz Sweetheart’Wema Sepetu na hatimaye kumuweka ndani kama mke wake.
“Naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kuwa kweli, sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja, naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake, nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu, ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini, kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia… One day you will be mine Wema Sepetu”, ameandika Harmorapa.
>
No comments: