BONGO MUVI WATOA SOMO LA USHOGA KWA WANAFUNZI
Wamama wa Bongo Muvi kupitia Malezi Daima Foundation leo wamefanya semina kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Buza jijini Dar, kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa kike na kiume shuleni na mitaani ikiwemo suala la kujiingiza kwenye ushoga na usagaji.
Akizungumza na GPL Mwenyekiti wa Malezi Daima, Foundation, Farida Sabu ‘Bi Sonia’ amesema kuwa, kama wazazi wameamua kujitolea kuelimisha watoto wao kuanzia ngazi ya shule ili kuwaepusha na vishawishi vya wanaume na wanawake ambao wamekuwa wakiwataka vijana wadogo ili kuwatumia. Kuepuka matumizi ya dawa za kulevya, mimba za utoto, ndoa za utotoni, masuala ya ushoga na malezi bora katika familia.
“Kama wa mama wa Bongo Muvi tumeamua kutoa elimu kwa watoto wetu waliko mashuleni ili kuwanuthuru na mimba za utoto, ndoa za utoto, matumizi ya dawa za kulevya, usagaji, ushoga na malezi mabaya nje na ndani ya shule.
“Hadi sasa tumeishatembelea shule zaidi ya tano jijini Dar es Salaam na mikoani, lengo letu nikuwafanya wanafunzi wawe na malezi bora nyumbani na shuleni.”alisema
Taasisi ya Malezi Daima inaundwa na wasanii wengine Asha Boko, Natasha, Bi Staha, Herieth Chumila, Grace Mapunda, Da Njaidi, Mama Mjata, Mama Nyamayao, Bi Fety na wengineo.
Aidha, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Buza, Bw. Joseph amewapongeza wamama hao kwa kujitoa kuwasaidia katika kudumisha na kuendeleza malezi bora kwa wanafunzi wao.
>
No comments: