BREAKING NEWS: AJALI MABAYA YATOKEA MOROGORO MAGARI MAWILI YAMEGONGANA WATU 4 WAFARIKI PAPO HAPO NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA WAKIMBIZWA HOSPITALI

Magari mawili yamegongana uso kwa uso katika barabara ya Morogoro Iringa maeneo ya Sangasanga na kusababisha vifo vya watu 4 na wengine majeruhi.Kamanda wa Zimamoto wa Mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na zoezi la kuwanasua majeruhi linaendelea
Picha na Maktaba
Muendelezo….
Ajali imetokea saa nane za usiku kati ya Fuso kutoka Iringa na Lori aina ya MAN la mafuta kutoka Dar
Fuso ilikuwa na dreva, konda na mwanamke mmoja ambao wote wamefariki papo hapo na Lori la mafuta dreva wake amefariki naye papo hapo.
Chanzo: TBC Taifa Redio.
>

No comments: