CHADEMA Achaneni na Watu Waliokula Wakasaza CCM Jikiteni Katika Kuibua na Kujenga Vijana Vyuoni na Ndani ya Chama

Hivi karibuni tumeona kuna utaratibu wa viongozi na vijana wa CHADEMA kwa ujumla kushangilia na kuona ni jambo la kheri kwa upinzani kupata wanachama wapya kutoka CCM na kwenda CHADEMA. Jambo hili sio kwamba ni baya hapana hata kidogo ni jambo jema kwa ukuaji wa demokrasia lakini naona ukakasi katika ujenzi wa chama.

Ukweli ni kuwa hawa viongozi waandamizi wanaohama kutoka CCM walikua na nyadhifa na madaraka makubwa Mfano Mawaziri Wakuu Sumaye na Lowasa,kuna Mawaziri Mfano Masha,Nyalandu na Makongoro Mahanga tunaona wengi wao wanakuja upinzani hasa CHADEMA wakiwa na malengo yao ya kisiasa au wakiona wameshindwa kutimiza malengo yao wakiwa CCM wanaona njia rahisi na kukimbilia CHADEMA hapa tupime baada ya nia yao kushindwa kutimia je nguvu na uwezo wao wa kukijenga chama uko kwa Namna gani?

Hapa nakishauli chama kijikite katika kuandaa makada hasa vijana vyuoni na ndani ya chama sababu hawa watakua na uchungu na chama hasa kukipigania na kukisukuma chama mbele mfano wa vijana walioibuliwa na chama vyuoni na mpaka leo tunaona michango yao katika kushawishi vijana wengine kuingia katika siasa mfano

John  Mnyika
Halima James Mdee
David Silinde
John Heche
Daniel Naftar Ngogo
Malisa Godlisten
Patrobas Paschal

Hawa ni baadhi ya vijana walioibuliwa na chama wakafundwa na chama na kukuzwa na chama nguvu yao tunaiona katika ujenzi wa Upinzani madhubuti na imara iwe ni kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Pili ni bora chama kikajikita ku recruit watu kutoka vyama vingne vya upinzani ambao watakuwa na manufaa katika ujenzi na kukipigania chama kuliko kuendelea kukumbatia hawa viongozi waandamizi kutoka CCM mfano CHADEMA kilipokea wanachama kutoka TLP na NCCR Mageuzi ambao mpaka leo tunaona impact yao ndani ya chama ni kubwa sababu wametoka upinzani ambako walikua wanapigania nchi wakaenda upinzani kwa wanakopigania nchi watu hao ni kama

Tundu Lissu
Peter Msigwa 
Godbless Lema
Mabele Nyaucho Malando 

Watu kama hawa mchango wao ni mkubwa na hauwezi kuulinganisha na mchango wa watu waliotoka CCM wakaja upinzani kama Sumaye,Masha na Kina Mkongoro Mahanga hii ni kutokana na ukweli kuwa hawa waliotoka CCM tayari wamekula wakashiba wakasaza sasa wanakuja kupumzika tu CHADEMA na kikubwa wameshika madaraka na nyadhifa kubwa za uwaziri na unaibu waziri ambapo wamekula kiapo cha kuto kutoa siri za baraza la Mawaziri na wakitoa ni kwenda kinyume na sheria ya usalama wa taifa so hata wakija hakuna wanalokuja nalo jipya ambalo tunaweza kulitumia dhidi ya CCM

Kama upinzani tunataka kupokea viongozi kutoka CCM tujikite katika kuwachambua na hata tunapowapa dhamana na kuwakaribisha na kuwashabikia wawe na sifa mfano vijana kama
Marehem Alphonce Mawazo ,
Esther Bulaya
Ally Bananga
Hawa ni vijana waliokuwa CCM na wakaja CHADEMA juhudi zao mpaka leo tunaziona katika ujenzi wa upinzani madhubuti.

Rai yangu CHADEMA tuachane na beba beba ya wanachama waandamizi kutoka CCM bali tujikitr kuangalia katika vijana wataoleta tija ndani ya chama 
>

No comments: