Enock Bella ajibu Maromboso kuzuiwa na WCB

Mwisho mwa weekend iliyopita kundi la Yamoto Band lilitumbuiza katika tamasha la Fiesta lakini msanii Maromboso hakuwepo, sasa Enock Bella amejibu kuhusu hilo.
Enock amekanusha uvumi kuwa Maromboso alizuiwa na uongozi wake wa sasa, WCB kuhudhuria show hiyo ambayo Aslay ndiye aliyewaita Enock na Beka Flavour jukwaani.
Muimbaji huyo ameendelea kwa kusema Maromboso alikuwa amesafiri kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kazi zake na si vinginevyo.
“Maromboso alikuwa amesafiri, halafu hawezi kukataa wala hizo ishu zisije zikawaumiza kichwa kwamba labada Maromboso amekataliwa kwenye uongozi wake au kakataa yeye mwenye kuja kufanya” Enock ameiambia Bongo5.
“Hapana yeye alikuwa amesafiri kwenda kufanya vitu vyake South Africa na yeye yupo katika maandalizi ya kuachia kazi yake mpya, kwa hiyo pia ingekuwa ngumu kumpata lakini kwa mara nyingine zote tutakua naye” ameongeza.
Enock Bella kwa sasa anafanya vizuri ngoma yake mpya ‘Sauda’.
>

No comments: