FAMILIA YA NDIKUMANA YAAMUA JUU YA MTOTO WAO

Familia ya marehemu Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu Tanzania, Irene Uwoya, imesema iko tayari kumsaidia mtoto wao aliyeachwa na marehemu Hamadi Ndikumana, Krish Ndikumana, ili kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa mcheza soka maarufu
mdogo wa marehemehu Hamadi Ndukaman, Laddy Ndikumana, amesema wao kama familia wako tayari kuhakikisha ndoto hiyo inatimia, kwani kipaji cha soka kipo kwa familia yao nzima.
“Tutajaribu kumsaidia kwa sababu kama familia nzima ni wanasoka, na hiyo ni kipaji ambacho yuko nacho tayari, tutamsaidia kufikia malengo yake”, alisikika Laddy Ndikumana akimwambia Big Chawa.
Marehemu Ndikumana ameacha watoto wawili akiwezo Krish ambaye amezaa na muigizaji Irene Uwoya, na aliwahi kusikika akisema nataka kuwa mcheza soka maarufu kama baba yake.
>

No comments: