HAYA NDIO MAAJABU YALIYOTOKEA KWENYE MECHI YA YANGA DHIDI YA SINGIDA UNITED

Idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Singida United dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Namfua ndio ndio maajabu pekee sana yaliyojitokeza katika mechi hiyo ukiachana na matokeo ya mchezo wenyewe ambao ulimalizika kwa suluhu.

Mashabiki wengi wa soka wa mkoa wa Singida na mikoa ya jirani (Tabora, Manyara, Dodoma, Shinyanga) kwa pamoja walijitokeza kushuhudia mchezo huu kutokana na timu ya Singida United kuonekana kuwa vizuri kwa kutengeneza kikosi chao vizuri lakini mabingwa watetezi Yanga wana mashabiki wengi katika ukanda huu.

Wingi wa mashabiki ukazidi uwezo wa uwanja wa Namfua, saa 6 mchana tayari majukwaa ya uwanja yalikuwa yamejaa hivyo mashabiki kuanza kusimama kutokana na miundo mbinu ya uwanja huo kutokuwa rafiki sana kwa sababu eneo la majukwaa ni dogo hivyo idadi kubwa ya mashabiki ilibidi wasimame au kukaa chini.

Muda mfupi kabla ya mchezo kuanza, mashabiki walizuiliwa kuingia uwanjani kwa sababu uwanja ulikuwa umejaa licha ya kiingilio kuwa 10,000 kwa jukwaa kuu na 7,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ni mdau mkubwa Singida United alilazimika kuwapanga mashabiki waliofurika uwanja wa Namfua ili wale ambao walikuwa nje wapate nafasi ya kuingia uwanjani.


Baada ya mageti kufungwa kufuatia uwanja kujaa, mashabiki waliobaki nje walilazimika kuushuhudia mchezo huo wakiwa nje ya uwanja kwa kupanda juu ya mlima wa mawe uliopo jirani na uwanja wa Namfua huku wengine wakipanda juu ya miti mirefu, paa na kuta za nyuma zilizopo kando ya uwanja.
>

No comments: