Lady Jaydee na Mwana FA uso kwa uso studio

Baada ya kurejesha ushikaji wao hivi karibuni ambao ulipotea kwa muda, hatimaye Mwana FA na Lady Jaydee wamerudi studio kufanya kazi.October 3 mwaka huu Mwana FA kupitia mtandao wake wa Instagram aliposti video ya wimbo mpya wa Lady Jaydee ‘I Miss You’ kitu kilicholeta shauka kwa mashabiki wa pande zote mbili kutaka kujua baada ya ushakaji huo kurudi iwapo watafanya tena kazi.
Sasa leo November 16, 2016 Lady Jadee ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa studio za B Hit’s na Mwana FA na kuandika; Last night Muziki, bila shaka kuna kazi ya pamoja inakuja.

Lady Jaydee na Mwana FA wameshaweza kutoa hit songs kama Hawajui, Msiache Kuongea, Alikufa kwa Ngoma na Wanaume Kama Mabinti bila kusahau ngoma walioshirikishwa na Ngwea ‘Sikiliza’.
>

No comments: