LULU AIBUA BALAA GEREZANI, MASTAA NI VILIO TU
Staa ‘grade one’ wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ (katikati). Picha na Maktaba.
Habari kubwa iliyojiri mapema wiki hii ni kuhusu hukumu ya kifungo cha
miaka miwili jela inayomhusu staa ‘grade one’ wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwigizaji mwenzake, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’.
TUJIUNGE GEREZA LA SEGEREA
Mara baada ya hukumu hiyo, mapokezi ya Lulu yalidaiwa kuzua balaa katika
Gereza la Segerea jijini Dar kwa wafungwa wenzake ambao walipigwa na
butwaa kusikia staa huyo ameingia gerezani hapo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ambaye alikuwa mahabusu siku ya Jumatatu
wakati ‘difenda’ lililombeba Lulu mara baada ya hukumu hiyo katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mrembo huyo aliibua tafrani
kutokana na kila mfungwa kutaka kumuona kwa mara nyingine.
ALISHASOTA SEGEREA
Ikumbukwe kuwa, Lulu alirejeshwa kwenye gereza hilo kwa mara nyingine
baada ya kukaa hapo kwa zaidi ya miezi nane alipokuwa mahabusu mara tu
baada ya kutokea kwa kifo cha Kanumba kabla ya baadaye kuachiwa kwa
dhamana. Shuhuda huyo alieleza kwamba, wakati akiingizwa gerezani hapo,
wafungwa hao waliacha shughuli zao kwa muda wakitaka kumuona na
kumshangaa Lulu kabla ya kuamriwa kuendelea na shughuli zao.
“Lulu ni staa mkubwa, kama ambavyo huwa watu wanamshangaa anapokuwa
mitaani au kwenye shughuli mbalimbali za hadhara, ndivyo ilivyokuwa
gerezani, lakini walitulia baada ya kuamriwa kuendelea na majukumu yao
na Lulu kuingizwa sehemu aliyotakiwa kwa ajili ya kukamilisha taratibu
za kuwepo kwake gerezani hao,” kilitiririka chanzo hicho.
NENO LA KAJALA
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya hukumu hiyo, staa mwenzake wa
sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ aliyewahi kukaa naye mahabusu
gerezani hapo alisema kuwa, anamhurumia Lulu kwenda mahali hapo kwa
namna maisha ya gerezani yalivyo. “Jamani hakuna kitu kibaya kwa
mwanadamu kama kunyimwa uhuru kama ilivyo kukaa gereza.
Hakika Lulu amekwenda pabaya, ninamsikitikia mno kwa sababu mimi napajua
Segerea,” alisema Kajala aliyekaa Segerea kwa zaidi ya mwaka mmoja
alipokuwa akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi na
Takukuru baada ya mumewe, Faraji Agostino kukabiliwa na kesi ya
utakatishaji wa fedha.
MASTAA WAMLILIA
Mastaa wengine waliomlilia Lulu baada ya kupigwa mvua mbili gerezani ni
pamoja na Snura Mushi ambaye alisema amesikitishwa sana na hali
iliyomkuta muigizaji huyo. “Hili siyo tukio la kufurahisha, lakini ndiyo
hivyo hatuwezi kushindana na sheria, iliyobaki ni kumuombea tu kwa
Mwenyezi Mungu ampe wepesi wa kila jambo,” alisema.
Kwa upande wake, Shamsa alisema; “Lulu ni mdogo wangu, msichana
mwenzangu na msanii mwenzangu, katika maisha kila jambo lina changamoto
zake, lakini kila kitu kitapita, tunamuombe Mungu ampe wepesi,
tutaendelea kumpa kampani, tutakuwa tunaenda kumtembelea mara kwa mara,” alisema.
tutaendelea kumpa kampani, tutakuwa tunaenda kumtembelea mara kwa mara,” alisema.
Mahsen Awadh maarufu kama Dk Cheni naye alionyesha masikitiko yake kwa
tukio lililomkuta msanii mwenzake, na kusema jambo hilo siyo dogo,
ingawa wapo watakaofurahi na kuhuzunika. “Hili siyo jambo la kufurahia,
hakuna mtu anayeijua kesho yake, haya ni mapito na yote tumwachie
Mwenyezi Mungu,” alisema.
Mastaa wengine waliotoa maneno ya huzuni kufuatia hukumu hiyo ni Wastara
Juma, Wema Sepetu na wengineo kibao. Wakati huohuo, msanii Hamisa
Mabeto ambaye amezaa na mpenzi wa Lulu, aliwashangaza wengi kwa kuongoza
maombi baada ya kuandika katika akaunti yake ya Instagram maneno ya
kumfariji Lulu, akimuomba Mungu kumsimamia na kumtia nguvu. “Mwenyezi
Mungu ampe nguvu mama yako na mdogo wako Iki katika kipindi hiki, sijui
kama nitaweza kumuona bila kutoa machozi, haya yote ni mapito tu,”
aliandika Mobeto.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kifo cha Kanumba kilitokea Aprili 7, 2012, nyumbani kwake, SinzaVatican
jijini Dar na mazishi yake kufanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni. Lulu
ndiye mtu wa mwisho aliyekuwa na marehemu chumbani kwake na ndiye
aliyewaita watu wengine baadaye. Wakati tukienda mitamboni, Wakili wa
msanii huyo Peter Kibatala aliyekuwa akimtetea, alisema atakata rufaa
Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu hiyo.
NA MWANDISHI WETU | RISASI JUMAMOSI
>


No comments: