LULU AKIWA GEREZANI TANGU AHUKUMIWE KIFUNGO CHA MIAKA 2 JELA,MDOGO WAKE KANUMBA NAYE AIBUKA NA HILI TENA

WIKI chache baada ya muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kufungwa jela, mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aitwaye aliyekuwepo siku ya tukio la mauaji hayo, hana mpango kwa sasa wa kwenda kumjulia hali msanii huyo gerezani.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Seth alisema hajapanga kwenda kumuona Lulu, lakini si kwa vile ana kinyongo naye bali kwa vile amebanwa na mambo yake mengi hivyo ni vigumu kupata nafasi.
“Sina mpango na sijapanga kwenda kumuona Lulu kwa kweli maana kazi zinanibana sana hivyo muda wangu ni mdogo, nina kazi za watu nyingi sana, Lulu yupo tu na siku nikipata nafasi nitaenda,” alisema Seth.
>

No comments: