MAGONJWA YANAYOWEZA KUMPATA LULU AKIWA JELA,DAKTARI AELEZA KWA UNDANI,ATAJA PIA MATATIZO MENGINE

Daktari wa magonjwa ya binadamu, Dk Godfrey Chale, akizungumzia hali ya Lulu baada ya hukumu hiyo alisema kuwa, kuna magonjwa ambayo huweza kumpata mtu mwenye matatizo ya kimaisha ikiwemo kufungwa jela ikiwa ni pamoja na kuwa kichaa kutokana na msongo. Dk Chale alisema mara nyingi watu ambao hupatwa na majanga makubwa kama la Lulu, huwa kwenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na msongo ambao husababisha mpangilio mbovu wa homoni kiutendaji na mhusika kuchanganyikiwa endapo atashindwa kukubaliana na mazingira ya tatizo.


         Alisema kuchanganyikiwa kwa watu wenye matatizo kama ya Lulu, hutokana na kuzidiwa na huzuni na mgandamizo wa hisia (depression) hivyo kushindwa kabisa kuzuia mfumo wa kufikiri na kutafakari na ndiyo maana unakuta mtu anaongea peke yake au kufanya vitendo vya ajabu kama kuokota vitu mbalimbali kama sehemu ya kujifariji na hapo ndipo tatizo la kuchanganyikiwa huanzia.


     Tatizo kubwa jingine ambalo linaweza kumpata Lulu ni kupoteza popularity momentum (nguvu ya umaarufu) na kushuka kwa uchumi atakapomaliza kifungo kwani kwa kipindi ambacho yuko jela atapoteza mikataba yake ya kikazi kama matangazo na uigizaji, vitega uchumi ambavyo vilikuwa vikimuingizia kipato cha kuyaendesha maisha yake.
chanzo 2jiachie
>

No comments: