MBEYA CITY WAIPA ONYO KALI TIMU YA SIMBA
Leo Jumapili katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Timu ya Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Simba lakini tayari wageni hao wamepewa onyo kuwa ni lazima waache pointi.
Hayo yamesemwa na mshambuliaji mwenye nguvu katika kikosi cha Mbeya, Mohammed Mkopi ambaye aliongeza wala hawana presha dhidi ya wapinzani wao hao na kwamba wanawaona ni wa kawaida tu kama timu nyingine.
“Maandalizi yetu yako vizuri na kila mtu ameupania huo mchezo ili tuwazibe midomo wale wote wanaotubeza huko mitaani na tunaamini tutafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi hii kwani Simba ni wa kawaida tu,” alisema Mkopi. Mara ya mwisho Mbeya ilifungwa na Simba mabao 2-0 uwanjani hapo.
>
No comments: