Rich Mavoko na Lulu Diva Wanaswa Kwenye Mahaba Mazito

Lulu Diva, Rich Mavoko Wanaswa Kwenye Mahaba Mazito
Mwanamuziki Lulu Diva amenaswa na msanii mwenziye Rich Mavoko wakiwa katika pozi za kimahaba usiku mnene katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam kwenye shoo ya Fiesta hivi karibuni.

Rich Mavoko alitumia udhaifu wa Lulu na kuanza kumshikashika maeneo mbalimbali ya mwili wake ambaye aliona raha na vicheko kedekede.  Mrembohuyo  hakujali kamera zilizokuwa zikimmulika ndani ya usiku huo mnene, kwani muda wote alikuwa bize akisikilizia mapapaso hayo bila woga.

Naye Mavoko aliyekuwa akimpapasa,  hakuwa nyuma katika kuhakikisha nafasi hiyo haipotei bila kutumika ipasavyo.

Huko nyuma wawili hao waliripotiwa kuwa wapenzi, jambo ambalo walilikanusha kila mara. 
 Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !
>

No comments: