Sababu za ukimya wa Batuli kwenye game


STAA wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema kuwa, anafurahi alivyokaa kimya kwa maana kufanya hivyo kunawafanya mashabiki wake wasimchoke na kummisi.
Batuli aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anaamini kabisa siku akiibuka na kitu chake chochote, kila mtu atakuwa na hamu nacho kwa sababu hawajamuona kwa muda mrefu.
“Mimi nafurahia sana watu kusema nimepotea hivi kwa sababu siyo kila wakati watu wajue mambo yako, wakuseme hovyohovyo, lakini ukiwa kimya kwa muda mrefu, ukiibuka, kila mmoja atakuwa na hamu na wewe,” alisema Batuli.
>

No comments: