Tembo wamjeruhi vibaya Mtoto wa miaka 13 Liwale.

Na. Ahmad Mmow, Liwale.
KUNDI la tembo lililongia na kupita katika kijiji cha Ngumbu, kata ya Kibutuka wilaya Liwale, mkoa wa Lindi limesababisha madhara. Baada ya mmoja wa tembo hao kumjeruhi vibaya mtoto Hemed Momboka(13) hapo jana.
Baadhi ya mashuhuda na ofisa mtendaji kata wa kata ya Kibutuka, Kelvin Msua walithibitisha na kuelezea tukio hilo. Mwananchi Hamis Mikdadi alisema mtoto huyo aliyekuwa na wenzake alifikwa na madhila hayo saa 4 asubuhi, baada ya kukutwa na kundi la tembo takribani nane, ambao walikuwa wanaelekea mto Mbwemkuru wakitokea upande wa kasikazini na kwenda kusini ambako upo mto huo.
Alisema mtoto huyo alirushwa mara tatu na hakuokolewa. Bali tembo huyo aliendelea na safari baada ya kuamini alishamuuwa. Nae ofisa mtendaji kata, Kelvin Msua alisema mtoto huyo alikutwa na kundi hilo la tembo nyumbani kwa babu yake ambako ni karibu na kijiji cha Ngumbu. “Babu yake Hemedi alikuwa analima, shamba lake lipo katika kitongoji cha Amani, kijiji cha Ngumbu. Hemedi alikuwa anacheza na wenzake, ghafla walitokea tembo, kwabahati mbaya Hemedi na wenzake wadhani ni ng’ombe wakawasogelea ndipo alipokamatwa na kurushwa takribani mara tatu,” alisema Msua.
Ofisa mtendaji huyo ambae kwakutumia gari yake alimsafirisha mtoto huyo kutoka kituo cha afya cha Kibutuka kumpeleka Liwale ambako ipo hospitali ya wilaya, alisema mtoto huyo alivunjwa uti wa mgongo na kutobolewa tumbo. Hali iliyosababisha sehemu ya utumbo kuwa nje ya tumbo.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Liwale, Dkt Kasanga Evarist Benito licha ya kukiri kumpokea majeruhi huyo, alisema; “Nikweli amejeruhiwa tumboni na uti wa mgmgo, hali yake sio mzuri anamajereha makubwa. Madaktari bado tunapambana kuokoa uhai wake”.
Juhudi za kumpata mkuu wa idara ya maliasili na maendeleo ya ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale zilishindwa. Baada ya kutokuwa hewani alipokuwa anapigiwa simu. Kwamujibu wa Msua, msako dhidi ya tembo hao unaendelea leo.
No comments: