TUNDA ANATAMANI INSTAGRAM IFUNGWE

VIDEO Queen mwenye visa lukuki Bongo, Tunda Sebastian anadaiwa kuwa na vitimbi vingi. Wiki iliyopita alijaa kwenye kumi na nane za Ijumaa Wikienda ambalo halikuchelewa kumweka mtukati ambapo alifunguka kuwa, ili uweze kukokaa kiakili hadi umri ni lazima kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za kwenye mitandao ya kijamii.
Muuza nyago huyu amefunguka mambo mengi juu ya maisha yake na kuhusu sakata la ujauzito wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, yule aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Over ze weekend: Mambo vipi Tunda? Mara kadhaa umedaiwa kunasa mimba na kila wakati kunakuwa na utata, ni kwa nini inakuwa hivyo?
Tunda Sebastian akifanya yake.
Tunda: Kiukweli hata mimi huwa naona watu wanaizungumzia tu mimba, lakini sina.
Over ze weekend: Lakini kwa nini mara nyingi picha zinakuonesha una mimba lakini baadaye huyeyuka?
Tunda: Mimi ninaona labda wanazitengeneza maana mimi sina mimba kabisa.
Over ze weekend: Vipi kuhusu ndoa yako na mpenzi wako Sabri maana ulisema mnatarajia kufunga pingu za maisha?
Tunda: Unajua unaweza kusema kitu, lakini mbeleni mambo yakaenda ndivyo sivyo.
Over ze weekend: Kwa hiyo mmeshaachana?
Tunda: Hilo bado sitaki kuliweka wazi kwa sasa.
Over ze weekend: Mara nyingi watu wanasema huna sehemu maalum ya kukaa na unapenda sana kukaa hotelini, je, hili unalizungumziaje?
Tunda: Sasa mimi nitakuwa mtu wa aina gani wa kukaa mahotelini maana pia si hela inatumika? Mimi nina kwangu, ninaishi Mbezi Beach, nikienda hotelini ni kwa ajili tu ya kubadilisha mazingira.
Over ze weekend: Mara nyingi unaonekana ni mtu wa kula bata sana, tena viwanja vya bei mbaya, unapata wapi fedha za kufanya matanuzi hayo huku ukiwa huna kazi?
Over ze weekend: Unajua Bongo watu wengi wanapenda mtu akiwa anafanya kitu, lazima mitandao ijue, mimi nina ishu zangu zinaniingizia pesa.
Over ze weekend: Vipi kuhusu skendo ya kutumia madawa ya kulevya?
Tunda: Unajua mtu ambaye anatumia madawa unamuona tu hata kwa kumuangalia, lakini hata ukiniangalia mimi sifanani kabisa.
over ze weekend: Kuna ishu iliwahi kusikika kuwa mke wa mwanamuziki Jose Chameleone alishatua Bongo kwa ajili ya kukusaka, kisa mume wake, vipi ishu hiyo ilikuwaje?
Tunda :(kicheko) hiyo sipendi kuizungumzia kabisa.
over ze weekend: Wazazi wako wanachukuliaje wanapokuona ukikumbwa na skendo mbali-mbali mitan-daoni?
Tunda: Unajua wale ni wazazi wangu, wananijua vizuri mtoto wao, kwa hiyo wakisikia vitu tofauti, hawawezi kunichukulia kwa hasira au kuvipokea moja kwa moja kwa vile wananijua.
Over ze weekend: Kuna kipindi ulikuwa umeamua kurudi shule, vipi umeshamaliza?
Tunda: Ndiyo, nilishamaliza nilichokuwa ninakisomea.
Over ze weekend: Ni kitu gani ambacho unakitamani kwa sasa?
Tunda: Yaani ninatamani siku moja Instagram ifungwe maana watu wote maisha yao ni kule na wanaweza kuyachambua maisha ya mtu kupitia kule kumbe wala siyo sehemu sahihi ya kumjua mtu alivyo.
Over ze weekend: Zamani uliwahi kukumbwa na skendo ya kupiga picha za utupu, vipi hiyo tabia umeacha?
Tunda: Jamani hivyo vitu vilikuwa zamani na ilikuwa ni utoto tu, sasa hivi siwezi kufanya hivyo.
Over ze weekend: Ninakushukuru sana Tunda.
Tunda: Karibu tena!
Stori: Imelda Mtema
>

No comments: