Yanga: HAWA HAPA WACHEZAJI WA YANGA WATAKAOIKOSA MECHI YA LEO DHIDI YA PRISON
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano klabu ya Yanga Dismas Ten amefunguka hali ya kikosi chao na wachezaji ambao watakosekana kwenye Mchezo kati ya Yanga na Tanzania Prisons waliosafiri kutoka jiji la Kijani Mbeya.
Dismas Ten ambaye ni moja kati ya Maafisa habari makini amesema Wachezaji wote wako fiti na mchezaji ambaye atakosekana ni Donald Ngoma Pekee.
Nimeongea na daktari wa wetu Dr Edward Bavy amenithibitishia kuwa wachezaji wote wako vizuri, Mchezaji pekee ambaye tutamkosa katika mchezo wa leo ni Donald Ngoma.
Licha ya wachezaji wengi kupona lakini Kuna uwezekano wachezaji kama Kamusoko, Tshishimbi wakaendelea kukaa benchi kutokana na kukosa Match Fitness Na hii ni kutokana na kutoshiriki kwa kiasi kikubwa kwenye mazoezi ya wiki hii.
>
No comments: