ANGALIA MATUKIO10 YALIOTIKISA MWAKA 2017,DIAMOND PLATINUMZ NA HAMISA WATAJWA,NDOA YA DOGO JANJA NA UWOYA,YUMO PIA LULU

Mwaka 2017 ndio huo upo ukingoni, kuna mambo mengi ya kujivunia, kusherekea, kuhuzunisha, kukatisha tamaa, kutia moyo nakadhali, yote ni sehemu ya maisha. Muziki/burudini ni sehemu ya maisha pia na kwa mwaka huu mzima kuna mengi wamejiri. Kwa upande huu pia kuna mazuri na mabaya yalitokea, Bongo5 tunakuletea matukio 10 yaliyotikisa vilivyo katika upande wa burudani kwa mwaka huu. Babu Seya na Papii Kocha kutoka jela December 9 mwaka huu wakati Tanganyika ikihadhimisha miaka 56 ya Uhuru, Rais Dkt. John Magufuli alitoa msahama kwa wasanii Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na baba yake Nguza Viking ‘Babu Seya’ waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela. Mwaka 2004, Babu Seya na wanaye walihukumiwa kifungo cha maisha jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi, pia mwalimu aliyetajwa kwenye kesi hiyo aliachiwa huru baada ya mashitaka dhidi yake kukosa msingi wa kisheria na vielelezo. Mwaka 2009, mahakama ya rufaa iliwaachia huru Mbangu (Nguza Machine) na Francis baada ya kujiridhisha kuwa hawakuwa na hatia. Babu Seya na Papii Kocha waliendelea na kifungo cha maisha baada ya kujiridhisha kuwa kweli walitenda makosa. Msamaha wa Rais ambao umewatoa Papii Kocha na Babu Seya ni kitu ambacho kimepewa nafasi kubwa ya mjadala miongoni mwa wapenzi wa muziki hasa dansi pamoja vyombo vya habari vya ndani na nje. Kutekwa kwa Roma Usiku wa kuamkia April, 6 kulianza kusambaa kwa taarifa za msanii Roma, Moni na producer Bin Laden kutekwa na watu wasiojuilikana wakiwa katika studio za Tongwe Records. Tukio hili liligonga vilivyo vichwa vya habari kwa vyombo vya habari kwa hapa Tanzania na nje ya nchi ukiachilia mbali harakati mbali mbali zilizokuwa zikiendelea katika mitandao ya kijamii ‘FreeRoma’. Kwa uzito wake haikuwa ajabu kusikia/kuona wabunge kadhaa na mawaziri wakisimama bungeni na kulizungumzia. Baada ya hayo yote hatimaye Roma na wenzake walipatikana wakiwa hai ingawa walikuwa na majeraha mbali mbali katika miili yao. Roma akaja akatoa ngoma yake ya kwanza ‘Zimbabwe’ tangu kutokea kwa tukio hilo na maisha mengine ya kimuziki kuendelea. Lulu kufungwa jela November 13 mwaka huu muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa muigizaji mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia. Akisoma hukumu hiyo Jaji Sam Rumanyika alisema kuwa mshtakiwa alijikanganya kipindi akitoa ushahidi wake mahakamani kitu ambacho hata kama marehemu angefufuka mahakama hiyo isingeliweza kupokea ushahidi wa marehemu. Baada ya kutoa maelezo hayo Jaji Rumanyika alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ambapo mawakili wa mshtakiwa walipewa muda wa kumtetea mshtakiwa mbele ya mahakama. Kesi ya Lulu ilianza kunguruma tangu mwaka 2012 ambapo ndipo kifo cha Kanumba kilitokea na mwaka 2013 alitoka kwa dhamana hadi pale ilipokuja tena kusikilizwa mwaka huu na hukumu kutolewa. Rais Magufuli amtoa Nay Polisi March 26 mwaka huu Nay wa Mitego alikamatwa na polisi akiwa Morogoro ikiwa ni siku chache tangu kutoa ngoma yake ‘Wapo’ ambayo ilikuwa inakosoa baadhi ya mambo serikalini. Baadaye Nay alihamishiwa kituo kikuu cha polisi Dar kwa mahojiano zaidi, wakati hayo yote ya kiendelea Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) tayari lilishaufungia wimbo huo. Kilichokuja kufanya tukio hilo kuwa kubwa na gumzo ni pale Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliposema kuwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Nay wa Mitego na kutakiwa auboreshe zaidi wimbo huo kwa kuwa umegusa masuala muhimu. Ishu ikaishia hapo. Diamond kuzaa na Hamisa Mwaka jana Diamond alimshirikisha Hamisa Mobetto katika video ya ngoma yake ‘Salome’ ambayo Hamisa alikuwa ni queen video. Baada ya Hamisa kubeba ujauzito drama zikaanza kuwa ujauzito huo Diamond ndiye anahusika. Baada ya Hamisa kujifungua drama zilifuata hapo si za kitoto, wakati Diamond akisistiza hausiki na ujuzito wa Hamisa, mrembo huyo alijitahidi kuweka wazi kuwa mtoto huyo ni wa Diamond. Moja ya njia alizotumia ni pamoja jina la mtoto kufanana na la Diamond na mwisho kulivuja picha zikionyesha wakiwa wote kitandani. Septeber 19 katika mahojiano na Clouds Media Diamond alikiri kuzaa na Hamisa na kueleza tukio hilo lilitokea kwa bahati mbaya ila alimueleza Hamisa kuwa yeye ni baba familia hivyo jambo hili liwe siri kati yao kitu ambacho kinaonekana kilimshinda mrembo huyo wa miss XXL mwaka 2009. Kilichofanya stori hii kuwa kubwa zaidi ni pale Diamond aliposema baada ya Hamisa kubeba ujauzito alimnunulia gari aina ya Rav4 na kutoa sh. milioni. 7 na laki 5 ili kumpeleka hospital ya Private kwa ajili ya kujifungua. Wasanii kashfa dawa za kulevya Mwaka huu RC wa Dar es Salaama, Mhe. Paul Makonda alitoa orodha ya wasanii waliokuwa wakidaiwa kujihusisha na matumizi pamoja na biashara ya dawa za kulevya. Ni kitu ambacho kilishtua sana kwani hakuna aliyetengemea na ni kitu ambacho hakikuwahi kufanyika hapo awali. Wasanii ndio kundi la mwanzo kabisa kutajwa na kiongozi huyo kabla ya wanasiasa/viongozi na wafanyabiashara kutajwa pia. Miongoni mwa wasaniio walitajwa ni pamoja na TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda, Mr. Blue, Vanessa Mdee, Wema Sepetu na wengine. Baada ya upelelezi kuna ambao alibainika kutokuwa na hatia na kuachiwa huru na wengine kama Wema Sepetu na Agnes Masogange kesi zao bado zipo mahakamani. Wema Sepetu na vyama vya siasa Mwaka huu Wema Sepetu amekuwa sana kwenye headline za siasa sana na hii ni kutokana na kuhama vyama vya siasa. February 24 alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM), hii likuwa ni siku kadhaa baada ya kutajwa katika orodha ya wasanii waliokuwa wakituhumiwa kutumia/kuuza dawa za kulevya. “Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama chama cha Mapinduzi na hivi sasa nataka kuhamia Chadema. Sitaki ionekane nimepata hasira kulingana na hizi tuhuma ambazo zimenikabili, nataka nionekane nimefanya maamuzi kama binadamu yeyote” alisema. Hata hivyo December Mosi mwaka huu alitangaza kurudi CCM na kuipiga chini Chadema kitu kilichomfanya kuonekana kama hana msimamo. Moja ya sababu alizotaja kuondoka Chadema ni madai kuwa hawezi kuendelea kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani. Rayvanny na ushindi wa BET June mwaka huu msanii kutoka label ya WCB, Rayvanny alishinda tuzo ya BET katika kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act. Ushindi huo wa Rayvanny ulimfanya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kushinda tuzo hiyo. Wasanii ambao Rayvanny alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica). Tuzo hizo ambazo zilizotolewa mjini Los Angeles, Marekani katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny aliweza kukutana na wasanii wakubwa wa Marekani kama Jason Derulo ambaye mwanzoni walikutana nchini Kenya. Pia alikutana na mastaa kama Fat Joe, Chris Brown, Lil Wayne, Karrueche, Amber Rose, Dj Khaled na Future. Rayvanny kushinda BET haikuwa ushindi wake pekee yake bali Bongo Flava ndio maana wasanii karibia wote wakubwa katika Bongo Flava walijitokeza na kumpongeza. Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya July mwaka huu kulianza kuvuma tetesi za wawili hawa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi mara baada ya kudaiwa kuonekana jijini Mwanza wakiwa pamoja lakini wote wawili walikuwa wakikanusha hilo. Hatimaye Jumamosi ya October 25 picha zikaanza kusambaa mtandaoni kuwa wamefunga ndoa, usiri pindi wa ndoa yao kufungwa ni kitu ambacho kilileta mjadala mkubwa sana katika vyombo vya habari na mitandao. Usiri huo wa ndoa na kutohudhuriwa na watu wa karibu wa Dogo Janja kama Mama yake mzazi ni kitu ambacho kilifanya wengi kutoamini juu ya ndoa. Siku chache katika mahojiano na Clouds Media Dogo Janja alifunguka kila kitu kuhusu ndoa yake na Irene Penzi la Vanessa na Jux Mwishoni mwa mwezi June Vanessa Mdee alithibitisha kuchana na Jux kitu ambacho kiliwashtua wengi kwani kulikuwa hakuna dalili za hilo kutokea na couple yao bado ilikuwa na nguvu sana. Katika mahojiano aliyofanya Vanessa na kituo cha redio nchini Nigeria cha Soundcity alibainisha kila mtu anaendelea na maisha yake. Baada ya kauli hiyo Vanessa aliporudi Bongo alifanya interview nyingi sana akizungumzia hilo, hata Jux naye pia lakini kwa namna ya kuachana kwao ilikuwa tofauti kidogo kwa sababu kila mmoja alikuwa akimzungumzia mwenzake kwa mazuri. Wakati hilo likiendelea Vanessa akaachia ngoma ‘Kisela’ na Jux akatoa ngoma ‘Utaniua’ ambazo maudhi yake kwa asilimia kubwa zilikuwa zinazungumzia kile kilitokea kitu kilichowafanya kuendelea kuzungumziwa katika vyombo vya habari. Walitumia hilo katika kufanya show za Fiesta kwa kutoa burudia ya aina yake kwa mashabiki wao kwa ahadi ya kuja kurudiana. Hadi msimu wa Fiesta unamalizika Dar es Salaam wakarudia wakiwa juu ya jukwaa na sasa maisha mengine yanaendelea. Mwisho; Asante kwa kuifuatilia Bongo5 wakati yote hayo yakijiri na kutupa dhamana ya kukuhabarisha, kiapoa chetu ni kuwa mwakani tutafanya hivyo tena kwa ueledi zaidi.
>

No comments: