ANGALIA PICHA KUAGWA KWA MKUU WA MKOA MSTAAFU JOEL BENDERA
Mwili wa Bendera ukipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa. MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaongoza mamia ya watu waliojitokeza kumuaga aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars, Joel Bendera katika Viwanja vya Hospitali ya Lugalo jijini Dar ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Korogwe, Tanga.Waombolezaji wakiwa wenyehudhuni. Bendera aliyefariki Jumatano wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliwahi kushika nyadhifa tofauti serikali ikiwemo ili ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mbunge wa Korogwe Mashariki na Mjini na baadaye kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro na Manyara.Mwili ukiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya Tanga kuzikwa. Simanzi na majonzi vimetawala wakati wa kuaga mwili wa kiongozi huyo ambaye pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa na Kocha Mstaafu.Viongozi wa TFF wa sasa na wastaafu wakijadiliana jambo wakatiwa kuaga mwili huo.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa na waombolezaji wengine.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akipita kuaga mwili wa marehemu Bendera.Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiaga mwili wa marehemu.Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akiaga mwili.Msemaji wa TFF, Alfred Lucas akiaga.Mbunge wa Sengerema na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngereja akitoa pole kwa waombolezaji.Ndugu wa marehemu wakiaga. MUSA MATEJA/GPL.
No comments: