Diwani Mwingine aitosa Chadema na Kujiunga CCM
Diwani wa Chadema wa Donyomurwak wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Lwite Ndossi maarufu Nsonuu amejivua uanachama wa chama hicho.
Pia, amejiuzuru udiwani na ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa iliyotolewa na idara ya itikadi na uenezi ya CCM Jumanne Desemba 19,2017 imesema Ndossi ameeleza sababu za kujiunga na CCM ni kuwa kujiunga na watu wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.
No comments: