MTOTO WA MIAKA 17, ATIWA MBARONI KWA KUJIFANYA MWANAJESHI (VIDEO)

Kijana Said Selemani, mwenye umri wa miaka 17, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Fahari iliyopo Goba,   amekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kujifanya askari wa jeshi na amekuwa akilazimisha kupata huduma, kutambuliwa, kuheshimiwa na kupata fursa nyingine kama kusafiri bila kutoa nauli.
Akizungumza na waandisi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LazaroMambosasa, amesema kuwa kijana huyo amekamatwa na amekutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na bila woga alipokamatwa aliendelea kujitambulisha kama mwanajeshi, na kutaja kuwa anatokea kikosi cha 501 KJ.
“Alipobanwa zaidi na kutakiwa aeleze kuwa mkuu wake wa jeshi ni nani na alienda mafunzoni mwaka gani, alishindwa na baadaye kukiri tu kuwa ni mwanafunzi na sare hizo alizipata tu na anazitumia katika kutenda vitendo vya kihalifu, yeye pamoja na wenzake ambao tunaendelea kuwafuatilia.
“Kwa sasa yupo mbaroni, anaendelea kuhojiwa ili tuweze kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka, na katika hili pia nitoe onyo kwa wale wote wenye tabia ya kujifanya ni wanajeshi na kufanya vitendo viovu, kama unataka kuwa mwanajeshi zipo taratibu zifuatwe upimwe uwezo wako wa kuwa mwanajeshi na mwisho ule kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,”amesema RPC Mambosasa



Na Isri Mohamed/GPL
>

No comments: