SHILOLE SOON KUMZALIA UCHEBE KIDUME!

STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa, kwenye ndoa yake aliyofunga hivi karibuni, atamzalia mumewe, Ashiraf Uchebe mtoto mmoja wa kiume. Akizungumza na Star Mix, Shilole au Shishi Trump alisema, hawezi kusema kuwa hatazaa wakati tayari yupo ndani ya ndoa. “Natarajia kumzalia mume wangu kidume mmoja maana siwezi kuwa kwenye ndoa nikabanabana,” alisema Shilole. Shilole na Uchebe, wameisogeza mbele sherehe yao ya harusi iliyokuwa ifanyike Desemba 20 hadi Desemba 28, mwaka huu. Na Imelda Mtema, Dar.
>

No comments: