STEVE NYERERE: “Polepole wewe nani? CCM hujaiunda wewe”

Gumzo la sasa hivi ni kuhusu Mwigizaji Wema Sepetu kutangaza kurudi kwenye Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukaa CHADEMA toka February mwaka 2017.
Baada ya Wema kutangaza huo uamuzi mpya, Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole alisema CCM haina taarifa za Wema Sepetu kurudi na hata hivyo watu huwa hawarudi kwenye Chama kupitia mitandao.
Kauli hiyo imewafanya Watu mbalimbali maarufu kutoa maoni yao akiwemo Steve Nyerere alieandika “hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya
Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia” – Steve Nyerere
EXCLUSIVE AUDIO: “WEMA ABAKI HUKOHUKO” – POLEPOLE ……Bonyeza play hapa chini kumsikiliza
>

No comments: