Alikiba Kwenye Ngoma Mpya Kesho, Ni Colabo Ya Nani ?

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Alikiba siku ya kesho anatarijiwa kusikika katika ngoma mpya ambayo ameshirikishwa na Abdu Kiba.

Pengine Alikiba kusikika katika ngoma hiyo inaweza isiwe stori, ila stori ni kwamba ngoma hiyo ni kwanza kutoka katika label ya Alikiba ‘King’s Music’ ambayo hapo awali alitangaza ujio wake.

Ngoma hii inakuja miezi mitatu tangu tangu Alikiba alipotoa ngoma yake ya kwanza kwa mwaka huu ‘Seduce Me’ ambayo mikono ya producer Man Water ilihusika, hata hivyo ngoma hii mpya ambayo video yake imeongozwa na Hanscana producer Man water kahusika tena.
Hii siyo ngoma ya kwanza kwa Alikiba kufanya na Abdu Kiba, utakumbuka walishafanya ngoma kama Kidela, Kajiinamia na nyinginezo.
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa ! >

No comments: