BREAKING NEWS: MEYA UBUNGO AACHIWA KWA DHAMANA

Meya wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob (Chadema) ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa takribani saa 15 tangu jana Jumapili akidaiwa kutaka kupanga njama za vurugu baada ya matokeo ya udiwani wa Kata ya Saranga kutangazwa.Meya Jacob alikuwa wakala katika majumuisho ya uchaguzi wa Kata ya Saranga hivyo alikuwa anahusika katika uchaguzi uliofanyika jana katika kata hiyo.Jacob ambaye pia nidiwani wa Ubungo alikamatwa na polisi jana saa tano asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Mtakatifu Peter, Kimara ambapo amesema baada ya kuachiwa na polisi, Jacob amesema alipokamatwa alipelekwa vituo vya Mbezi kwa Yusuf, Mabatini na baadaye Oysterbay alikokaa muda mrefu.Nimeachiwa saa 7:40 usiku kwa dhamana, hizi zote zilikuwa ni njama za kutunyima ushindi. Dhamana gani inatolewa usiku? Hii ilikuwa mipango ili Chadema isishinde ila wakazi wa Ubungo wasivunjike moyo na haya, wamejionea hali halisi iliyofanyika na huu ni ushindi kwetu.” amesema Jacob.Meya huyo amesema ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay leo Jumatatu.
NA GPL
>

No comments: