DK. SHIKA KUONGEA NA WANANCHI DAR LIVE USIKU WA ITAPENDEZA
DK Louis Shika, ‘bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, anatarajiwa kuongea na wananchi, Desemba 9, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mratibu na meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’, alisema kuwa, kwa mara ya kwanza kuanzia saa kumi na mbili za jioni, Dk Shika ataongelea mabilioni yake yalio njiani kuja nchini, maisha yake ya zamani na sasa pamoja na mambo mengi aliyopitia.
“Wengi bado wapo njia panda kuhusiana na ukweli wa mabilioni ya Dk Shika. “Tumeona wiki mbili zilizopita amelipia bima fedha zake katika Shirika la Posta. “ Kabla fedha hizo hazijatua ameona atoe kwanza sapraizi kwa wananchi ambapo ukija Dar Live utaishuhudia,” alisema KP Mjomba.
-credit: GPL
>
No comments: