DK. SHIKA ADAI HAJIWEZI KWA RAY C
DAKTARI Louis Shika ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya jaribio lake la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, ametoa mpya baada ya kudai kuwa anaguswa na muziki wa mkongwe Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko juzikati, Dr Shika alisema katika Tanzania, hakuna msanii yeyote wa Bongo Fleva ambaye anamhusudu zaidi ya mwimbaji huyo anayesifika kwa kuimba na kucheza.
“Ukiniuliza ni msanii gani wa muziki wa Kitanzania ambaye namkubali, sipati kigugumizi kukuambia kwamba ni Ray C, kwake sijiwezi, napenda anavyoimba, anavyocheza na kadhalika, wimbo ninaoupenda zaidi ni ule uitwao ‘Nataka Niwe Nawe Milele’ wa msanii huyo,” alisema Ray C
Stori: Ally Katalambula.
>
No comments: