Dogo Janja Atumiwa Meseji Hii hapa na X wa Uwoya
Mwanamuziki na aliyewahi kuwa mpenzi wa muigizaji Irene Uwoya, Msami Baby amempongeza msanii mwenzake Dogo Janja kwa kufunga ndoa na muigizaji huyo huku akiwasifu kwamba wameweza kuwabadilisha watu kuhusiana na umri.
Msamii ametoa pongezi hizo leo kwenda kwa wawili hao baada ya Dogo Janja kukiri kwa kinywa chake kwamba tukio linaloonekana kwenye picha mbalimbali siyo kiki kama watu wanavyodhani bali ni ndoa kweli.
Msamii ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba "Ndoa ni jambo la kheri sana, pongezi kwako Dogo Janja na Irene Uwoya mmefanya watu wajue umri ni 'number' tu ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi" aliandika Msami
Msami aliwahi kuwa kwenye mahusiano na muigizaji Irene Uwoya ambapo karibuni alipokuwa kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa kila Ijumaa alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Uwoya alidai walishaachana na kudai kwamba Uwoya ndiye aliyemtongoza mpaka kufikia kuwa wapenzi.
>
No comments: