Msanii Mkongwe Ferooz Amalizwa na Madawa ya Kulevya....Mwenyewe Akana Kutumia
Msanii mkongwe wa bongo fleva aliyetamba miaka ya nyuma kidogo na nyimbo yake ya ‘Starehe’ iliyofanya vizuri sana amefunguka na kudai tuhuma zinazomkabili kuwa anatumia madawa ya kulevya sio za kweli hata kidogo.
Wasanii wengi waliokuwa wanafanya vizuri siku za nyuma huishia kuchukua njia mbaya na hivyo kuishia kujiingiza katika matendo maovu kama kuuza na kutumia madawa ya kulevya na hivyo kupelekea vipaji vyao kufa wengi wao hudai hujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu ya ugumu kwenye gemu mfano wa wasanii waliojiingiza kwenye madawa ya kulevya ni pamoja na Ray C, Chiddi Benzi.
Ferooz ni moja Kati ya wasanii ambaye kwa kipindi kirefu ametuhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya Kulevya ambayo ndio yamepelekea kupotea katika ramani na kuzidi kuwa kimya tuhuma ambaxo Ferooz amezikana kwa nguvu shutuma hizo na kudai kuwa taarifa hizo hazifai kuaminiwa na watu wanaozisambaza ni wale wenye nia ya kumchafua na wasio mtakia mema.
Sijawahi kutumia dawa za kulevya na kama kuna mtu anayeshupalia kitu hicho tunaweza tukaweka dau tuende tukaangalie tuhakikishe na kama natumia sawa atakua ameshinda na jamii itakuwa imejua na kama nitaonekana situmii basi niondoke na dau langu na jamii itakuwa imeshajua situmii kitu kama hicho”.
Pia msanii huyo alielezea nia yake ya dhati ya kutaka kurudi kufanya muziki hivi karibuni kwa kutangaza kuwa anategemea kutoa ngoma yake hivi karibuni. >
No comments: