FAIZA ALLY AFICHUA SIRI YA ATAJA SABABU ZA KUMUANIKA MZAZI MWENZIYE

MSANII wa filamu Bongo, Faiza Ally amesema kuwa, japo mwanzoni aligoma kumuanika baba mtoto wake lakini siku chache zilizopita aliamua kumueka wazi baada ya mwanaume huyo kuridhia. Akipiga stori na paparazi wetu, Faiza alisema, awali mwanaume huyo ambaye hakupenda kumtaja jina lake, alikuwa hataki kujulikana mitandaonilakini sasa ameridhia wamjue yeye ndio baba halali wa mtoto wake aitwaye Li na kufunika uvumi wa kwamba mtoto huyo ni wa baba mwingine. “Baba mtoto wangu mwanzo hakupenda watu wamjue, lakini maneno yamekuwa mengi mara nimezaa na Sugu (Joseph Mbilinyi) wengine wanasema Gabo (Salim Ahmed) wengine mwanaume mchina, jambo hilo limemkera akaona bora nimuweke wazi na jamii imjue,” alisema Faiza.
>

No comments: