MPIGA PICHA WA DIAMOND PLATNUMZ KIFESI AANDIKA UJUMBE WENYE FARAJA KWA LULU

By @kifesi – Dear Lulu …. Sisi wengine tulosoma boarding za enzi hizo tulikaa jela miaka sita kwenye shule za boarding za serikali! Tukila ugali mbichi wa dona na maharage yasiyo na ushirikiano tena yana wadudu harage lina funza wadogowadogo weupe na ili kupoteza ushaid tunayapondaponda maharage n funza wake vinakua kitu kimoja unakula freshii .na kama halina funza unakula harage kama unakula karanga afu maharage yametiwa mafuta ya taa eti kutupunguza nyege, ukija ugali umejaa nyuzi nyuzi,,siku nyama ikipikwa ni nyama ya wanafunzi 800 but inatiwa nyanya mbilli unakula kipande kimoja.. afu siku ya wali tunakula kwa majina kma hujamaliza fees unakula kwa macho… wali hauelewek n wali au kande hauna radha but ndio…

      tuliugombania…kulala kwa kengele na kuamka kwa kengele kwanza mnalalla kwenye kunguni .asubuhi sa 11 kuamshana mchakamchaka, Tulifanya kazi ngumu..kulima mashamba ya shule..kuchimba visiki..kubeba molamu or kokoto…kufyatua matofali kma adhabu plus masomo magumu ikiwa ni pamoja na kusoma vitabu vigumu vya mzungu kwa lugha isiyoeleweka wanaiita kiingereza..kuna kitabu kiliitwa KUSADIKIKA cha kiswahil lakin hakieleweki

..hapo bado viboko vya haja..unacharazwa kiboko had kinaishia matakon mwako na ukionekana unachungulia getin unaambiwa unatka kutoroka ila mwisho wa siku miaka 6 iliisha tukatoka. Hakuna marefu yasiyo na ncha Lulu. Cha muhimu kua strong, miaka miwili sio mingi kivilie! its better kukaa huko but uko huru na upweke wake kulikoni huku uraiani ambapo kila mtu anakutazama kwa jicho la mkosaji ..kukusakama na kukulaumu ….
atleast nafsi itakua huru kwa kulipa deni….
… alosoma boarding school za enzi hizooo n unakumbuka nn tukumbushane 😂😂 sema tulopitia maisha hayo yalitu shape tuwe strong leo hii tuna uwezo wa kuishi mazingira yoyote yale bila tabu kabisa hatuna umama mama.
>

No comments: