WEMA ATUPIA UJUMBE MZITO INSTAGRAM WA KIFO CHAKE
STAA wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, kupitia akaunti yake ya Instagram leo ametupia ujumbe mzito juu maisha yake ya sasa na kipindi atakachokuwa hayupo duniani. Mrembo huyo amesema kuwa kipindi atakachokuwa amefariki watu watakuwa wanamuongeleaje na kasema muda mwingine anaomba Mungu amchukue akijua kuwa anamkosea. Pia alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa anaomba kuwa mbali na mitandao ya kijamii.
Ujumbe aliotupia wema ni ufuatao:
Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele… Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema…” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu… Ya Duniya ni mengi sana…. Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist… Ila acha niendelee kumtegemea yeye… Kila jambo hutokea kwa sababu…. Hili nalo litapita… I think I need a Time Off Social Media… Kwa mara nyingine Tena…. Siwezi jamani…
No comments: