Yanga, Azam zamgombania Mdhamiru
Azam na Yanga ni wapinzani wakubwa wa Simba inaongoza ligi kuu ikiwa na pointi 23, zimefikia hatua ya ya kuwatuma watu wao wamfuatilie na kuzungumza na Mdhamiru ili atue kwao baada ya kugundua amebakisha muda wa miezi sita ambao unampa uhuru wa kufanya mazungumzo na timu nyingine yeyote.
Mtu wa karibu na jirani wa mchezaji huyo anayeishi Magomeni jijini Dar es Salaam alisema, anaona kila kitu kinachoendelea hapo na Simba wasipokuwa makini, ataondoka kweli.
"Niliwaona matajiri hao kwa nyakati tofauti nyumbani kwake,hata hivyo Mzamiru anaonekana akili yake anaielekeza nje, kuliko kucheza soka la Tanzania, lakini lolote linaweza kutokea si unajua pesa inaongea,"alisema jamaa huyo.
No comments: