Simba yasaka nyota wapya
Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma alisema pamoja na usajili mkubwa ambao Simba waliufanya wakati wa kipindi cha usajili wa mwanzo wa msimu huu, wataongeza baadhi ya wachezaji ili kuimarisha ufanisi wa kikosi chao.
"Kuhusu usajili ndio maana kukawekwa kipindi cha usajili wa dirisha dogo kwamba timu zinaangalia nafasi zipi zinahitaji kuimarishwa na nani wanaostahili kuongezwa. Ukiangalia Simba inakabiliwa na mashindano mengi msimu hu yale ya ndani pamoja na ya kimataifa.
Hivyo ni lazima tuhakikishe tunakuwa na kikosi kipana na imara ambacho kitaweza kushiriki mashindano yoye bila shaka yoyote. Kwa hiyo naamini tutafanya usajili," alisema Djuma.
Simba imekuwa ikihusishwa na usajili wa wachezaji Shazil Haimana, Mohamed Rashid pamoja na Hassan Kabunda.
No comments: