BABU SEYA, PAPII KOCHA KUTINGA IKULU!

Wakati wakianza wiki ya pili tangu waachiliwe kwa msamaha wa rais kutoka katika kifungo chao cha maisha gerezani, imebainika kuwa wanamuziki nyota nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ watatinga Ikulu ili kutoa neno la shukurani kwa Rais John Pombe Magufuli. HIVI NDIVYO ILIVYOANZA Msemaji wa familia ya Nguza, Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki, alifanya mahojiano marefu na Risasi Mchanganyiko na kuzungumzia mambo mbalimbali juu ya mipango ya wanamuziki hao ambao wanaonekana kuwa na mashabiki wengi. KUHUSU KUACHA AU KUFANYA MUZIKI King Kikii alisema kwa anavyofahamu yeye, ni lazima Babu Seya ataendelea na muziki kwa vile ni kazi iliyo ndani ya damu yake ambayo ameifanya kwa miaka mingi, hivyo suala la kuacha halipo kabisa. “Hata alipokuwa jela, tulimpelekea gitaa akawa anapiga, kwa sababu hajawahi kuwa na kazi nyingine, kwa hiyo nina uhakika anataendelea Nguza Viking ‘Babu Seya’ enzi akiwa magereza. ANAKUMBUKA NINI WALIPOTOKA JELA? “Ilikuwa ni furaha tu kubwa kwa kila mmoja, maana nilishangaa kukuta wingi wa watu siku ile. Hii inaonyesha jinsi gani wanapendwa. Lakini kitu ninachokumbuka vizuri ni kuhusu Papii, alinitambulisha kwa watoto wake wawili wa kike, wakubwa kabisa akisema ni wanae. LINI ATAPANDA KWA ONYESHO LA KWANZA? “Sijajua ni lini, lakini nadhani itakuwa ni onyesho moja kubwa sana na ili liende vizuri, ni lazima niwe naye, ili tuimbe zile nyimbo tupo Marquis, yeye aimbe za kwake na mimi niimbe za kwangu, itakuwa kitu kimoja kizuri sana. “Hii haitaki onyesho lifanyike ndani ya ukumbi, inatakiwa uwanjani kabisa, kama ni pale Uwanja wa Taifa au Uhuru, maana ninajua watu watakuja kwa wingi sana kutaka kupata burudani kutoka kwake. Rais John Pombe Magufuli. KUNA MPANGO WOWOTE WA KUTEMBELEA MIKOANI? “Ndiyo, tutatembelea mikoa yote mikubwa, Mwanza, Arusha, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Kigoma, lengo letu ni kutaka watoe salamu za shukurani kwa watanzania, kwa sababu namna walivyopokewa, ni jambo zuri sana. KUNA MPANGO WA KWENDA IKULU? “Mpango huo tunao, tutakwenda Ikulu kutoa mwaliko wa onyesho letu la kwanza tu, tungependa Mheshimiwa Rais Magufuli aje, kama atakuwa ametingwa na kazi zingine za kitaifa, basi hata atume mtu amwakilishe, tunataka kumshukuru kwa moyo wake wa kibinadamu, tunamshukuru sana kwa kweli. VIPI KUHUSU MAPROMOTA? “Watu wa kuibeba hii shoo wapo, kuna walioonyesha kuvutiwa na tumeshaanza mazungumzo ya awali ila bado hatujafikia muafaka, kitu cha msingi ni kutaka onyesho hili lifanyike kwa sababu lengo lake hasa ni kutoa shukurani zetu kwa watanzania, furaha waliyokuwa nayo wakati wameachiwa kutoka jela imetupa faraja sana,” alisema Kikii. DAR ES SALAAM:
>

No comments: