KAJALA MASANJA TENA,AZUA BALAA ZITO BARABARANI
Muigizaji mwenye ‘taito’ kubwa Bongo, Kajala Masanja amenaswa akipiga misele barabarani na kuzua gumzo la aina yake kutokana na nguo aliyovaa kumbana mwili kiasi cha kuonesha laivu ukubwa wa kalio lake. Tukio hilo lilishuhudiwa na paparazi wetu mapema wiki hii ambapo mrembo huyo alinaswa akikatiza mitaa ya Bamaga-Mwenge kuelekea Sayansi akiwa ameongozana na bwa’mdogo mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja. Watu waliokuwa kwenye magari yao binafsi walionekana kupunguza mwendo na kumfuatilia Kajala kwa karibu huku wale makondakta wakipiga miluzi kutokana na jinsi walivyopagawa na mrembo huyo. “Oyooo dah hawa watu nilidhani ni mambo ya kwenye TV kumbe ukiwaona laivu pia ni balaa,” alisikika konda mmoja aliyekuwa kituoni Bamaga. Paparazi wetu alimfuatilia hatua kwa hatua Kajala ambapo baadhi ya wenye magari binafsi walionekana wanataka kusimama kabisa, lakini walionekana kushindwa kufanya hivyo wakimhofia kijana ambaye aliongozana na Kajala. “Unaweza kukuta huyo mshikaji japo anaonekana mdogomdogo lakini anatoka na Kajala. Hawa mastaa hawashindwi hawa,” alisikika jamaa mmoja aliyekuwa akimkodolea macho Kajala. Njemba mwingine alisikika akisema kuwa; “Mh! Kajala huyu si yule wa mwanzo. Amebongeka sana. Kwa kweli hili umbo lake kwa sasa hastahili kutembea kwa miguu kama hivi. Huyu ni mtu wa kukaa kwenye gari muda wote.” Mwanahabari wetu aliendelea kumfuatilia Kajala kwa muda mrefu, lakini baadaye alibaini kuwa yupo mazoezini kwani alikuwa akienda na kurudi na hata alivyomshtukia paparazi wetu akimfotoa picha, hakutaka kuzungumzia lolote. Stori: Boniphace Ngumije, Amani
>
No comments: