KABLA YA 40 NDIKU,UWOYA ACHAFUA HALI YA HEWA!,MAZITO YAANIKWA LIVE

Hata kabla ya siku 40 baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ au ‘Ndiku’, staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya, anadaiwa kuchafua hali ya hewa na kuwafanya watu wake wa karibu kushindwa kuamini alichokifanya. Jana, Jumapili, picha za Uwoya akiwa kimahaba kitandani na mwanaume, zilichafua upepo kwenye mitandao ya kijamii ambapo mwanamama huyo alinangwa kuwa, angalau angesubiri mumewe huyo aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume, atimize siku 40 kaburini ndipo ajiachie.
Picha hizo zilisambaa wakati Ndikumana akitimiza mwezi mmoja na siku mbili tu kaburini kwani alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, mwaka huu akiwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Rayon ya Rwanda. Gazeti hili lilifanya uchunguzi juu ya picha hizo ambapo kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Uwoya, picha hizo zilisambaa ikiwa ni mwendelezo wa ‘kutafuta kiki’ ya tamthiliya mpya ya msanii huyo baada ya ile kiki yake na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ya kufunga ndoa kudaiwa kubuma. Jana, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ‘fizikali’ kwa kufika nyumbani kwake maeneo ya Sinza-Mori, Dar, lakini likamkosa. Alipoendewa hewani, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu STORI: Imelda Mtema, Dar
>

No comments: