Mbowe Fanya Tathimini Kuinusuru Chadema Kama Mwenyekiti Taifa, Wafuasi Mitandaoni Wamezidiwa

Ndugu mwenyekiti Freeman Mbowe kuna sehemu kama chama kikuu cha upinzani nchini tumekosea, nguvu ya chama inaendelea kupwaya.
Kama kiongozi mkuu jaribu kusikiliza maoni mbali mbali ya wanachama na wapenzi wenye nia njema ya kuona Chadema kinaimarika na kushika dola.

Kuendelea kuilaumu CCM badala ya kutafakari kwa kina wapi tumekosea hakutanusuru kuanguka kwa chama chetu.
Kwa mfano ajenda yetu kwa sasa ni ipi?, mbona wale tuliosema wachafu kwa miaka mingi tunawapokea na kusema ni wasafi ?, tatizo ni Nini?, usafi wao unakuwepo wakihamia upande wetu?

Je wananchi na baadhi ya wanachama wafia chama wanatuelewaje?

Mkuu mwenyekiti, Freeman Mbowe, bila tafakuri ya kina jahazi linazama pole pole , mitandaoni vijana tumebakiza matusi na kejeri, je ndo yataimarisha chama chetu?, wale vijana Mahili wajenga hoja na wachambuzi wa sera wako wapi siku hizi?.

Wakati ni Sasa, bado hatujachelewa, tubadili mbinu na mikakati ya kuimarisha Chadema

Angalizo, mbinu ziwe ni zile zisizo na madhara kwa raia na mali zao
>

No comments: