Shukrani ya Punda ni Mateke , Chadema Msikatishwe Tamaa

Mungu ibariki Chadema , chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele kuwarejeshea utu wao watanzania wenzetu wanaodhalilishwa kwa tuhuma za kutunga , Chadema imetumia mpaka Wanasheria wa chama kupangua kesi wanazotungiwa baadhi ya watanzania mahakamani kisiasa, Mungu aendelee kuwapa moyo huohuo na awajalie subira kuu.

Pamoja na kujitoa kwenu lakini baada ya kufanikiwa kurudisha Utu wao uliopondwa mithili ya karanga za kuungia kisamvu , baadhi ya wahanga wamekuwa na shukrani ya punda , hiyo isiwakatishe tamaa ya kuokoa wengine .

Endeleeni kuwapigania wengine wanaoonewa bila kuchoka , maana vitabu vya kumbukumbu vitawaandika , punda ana tabia ya kurusha mateke hata kama unamtoa mwiba kwenye mguu wake mwenyewe .

By Erythrocyte
>

No comments: