MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO APEWA KICHAPO HUKU AMEFUNGWA KWENYE MTI

 Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Sokoine, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ameshambuliwa na vijana wawili baada ya kumfunga kwenye mti na kumpa kipigo hali iliyomsababishia kupata majeraha mwilini.


Mtoto huyo anayeishi na bibi yake, mtaa wa KCMC Rau alipewa kipigo hicho leo Ijumaa baada ya bibi yake ayenaishi naye kudaiwa kutoa maagizo kwa vijana hao kufanya hivyo.


Shuhuda wa tukio hilo, Emanuel Shirima amesema kuwa mtoto huyo alipigwa baada ya kwenda kuogelea.


Amesema kuwa mtoto huyo sio mara yake ya kwanza kupewa kipigo na huyo bibi yake huyo.

"Yaani huyu mtoto ana kama mwaka hivi anapigwa na kunyanyaswa na huyu bibi," amesema shuhuda huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema hana taarifa yoyote.

Hata hivyo, Kamanda Issa amesema atafuatilia suala hilo kwa kuwa limetokea leo Ijumaa jioni .

Na Janeth Joseph, Mwananchi
>

No comments: