Ona Jinsi gani Mahusiano ya Kimapenzi yanavyomweka Mtu Pazuri Kimafanikio: Case study; Diamond vs Belle 9
Kwa kujadili hii maada nimependelea kwanza nioneshe historia japo kwa ufupi ya safari ya maisha kati ya hawa wanamziki wa Tanzania Belle 9 na Diamond tuone jinsi gani mmoja wao Mahusiano ya kimapenzi yalivyo ng'alisha juhudi zake kikazi na kufanikiwa na leo hii ni billionaire.
Kwa wasiojua Diamond na Belle 9 wote walitoka kipindi kimoja kama sijakosea mwaka 2009 hivi. Wote hawa walikuwa maunderground. Belle 9 akitokea Morogoro mji kasoro bahari pale mtaa wa Mafiga. Wengi walianza kutabiri kuwa kijana huyo mdogo ( Belle 9 ) alikuwa amekuja kujaza nafasi ya mkongwe na mwakilishi wa mziki mkoa wa Morogoro yaani Afande sele ambaye alikuwa ameanza kufifia kiutunzi na nyota pia.
Diamond yeye alitokea mkoa wa Dar es Salaam pale Tandale.
Wawili hawa wote walikuwa wadogo sana kiumri tuseme walikuwa under 20 na walitoka na ngoma kali.
Belle 9 yeye alitoka na ngoma iitwayo Sumu ya Mapenzi ngoma iliyomtambulisha vyema sana kwenye medani za mziki hapa tanzania. Ngoma hii ilikuwa imetulia ki melodi na saiti pia.
Diamond yeye alitoka na ngoma iitwae Nenda kamwambie wimbo ulomtambulisha nae pia vizuri kwenye medani za muziki hapa nchini.
Nakumbuka kipindi kile Radio Free Africa walikuwa na kipindi cha Mpambano wa wasanii ambao wanaimba mziki unaofanana na kuwashindanisha kwamashabiki walokuwa wakipiga kura kwa njia ya simu. Kipindi hiki kilikuwa pendwa sana na bora.
Siku moja walishindanishwa hawa wasanii ( Belle 9 na Diamond) na kura kutoka ngoma draw basi ilibidi mpambao huo urudiwe wiki inayofata ambapo Belle 9 alishinda kwa kishindo.
Mwaka 2010
Belle 9 alitoa ngoma nyongine iitwayo Masogange ambayo nayo pia ilikuwa kali sana na ilitikisa inchi nzima huku akijizolea umaarufu maradufu.
Diamond nae alitoa ngoma iitwayo Mbagala amabayo nayo vile vile ilitamba sana tena sana kutokana na maudhui mazuri na melodi iliyojaa ufundi. Nae pia kama ilivo kwa Belle 9 alizidi kujizolea umaarufu maradufu kwa watanzania ila hakumfikia Belle 9.
Mpaka hapa ambapo kila mmoja alikuwa ana single mbili mbili hit songs; Belle 9 alikuwa yuko juu kutokana kwamba watu wengi walikuwa wanamkubali sana yeye kutokana na kwamba ngoma zake ( Sumu ya mapenzi na Masogange) ziliweza kuwakosha nyoyo watanzania.
Baada ya muda Belle 9 aliachia ngoma nyingine iitwayo Wewe ni wangu au Wewe unanifaa ambayo pia ilimpaisha juu sana huyu kijana na wana Morogoro wakanyosha mikono wakisema kuwa sasa zile enzi za utawala wa Afande sele yule mkali wa Rhyms na Dogo Ditto wake zimeisha na sasa huyu dogo amekuwa Icon ya wana mji kasoro bahari. Dogo alitamba sana tena sana.
Diamond nae hakuwa nyuma; nae alitoa ngoa iitway Ntarejea ambayo nayo pia ilifanya viziri japo kuwa haikuifikia hiyo ya Belle 9 ( Wewe ni inanifaa)
Mpaka hapo Belle 9 alikuwa juu kweli ukimlinganisha na Diamond. Mtoto kutoka Moro alikuwa akitingisha kwa nyimbo zake hizo yaani Sumu ya mapenzi, Masogange na Wewe unanifaa. Diamond alikuwa hafui dafu hata. Hata kwenye fiesata 2010 Belle 9 alizidi kuwa kivutio sana
Si kuwa Belle 9 alikuwa akipendwa kwa hizo nyimbo tu na sauti yake bali hata sura; yeye alionekana kuwa baby face yaani handsome ukilinganisha na Dimond ambae yeye Sauti tu ndo ilikuwa ikimbeba ila kwa upanda wa sura ilikuwa shida!!! Belle 9 akivaa alikuwa akilipuka ile mbaya ila kwa mwenzangu na mimi Diamondi nguo zilikuwa zikimkataa kutokana na ukweli kwamba alikuwa na sura NGUMU!
Nakwambia kila hawa wasanii walipokuwa wakipambanishwa Belle 9 mtoto wa mji kasoro bahari alikiwa akiibuka kidedea!!
Nb: kwa kipindi hicho; hakukuwa na skendo yoyote ya kimahusiano ya Mapenzi kwa warembo mbali mbali kwa wasanii hao!
ZAMA ZA DIAMOND NA KUMPIGA GAP BELLE 9
Belle 9 baada ya kuwa na hizo hit songs na kuona kuwa yuko juu alianza kusua kusua kiutunzi huku mwenzake Diamond akikomaa na kukesha akitunga mashairi.
Diamond alituletea ngoma kama Binadamu; Kizaizai na Moyo wangu ambazo zilifanya vizuri sana hasa wimbo Moyo wangu ndo ulikuwa funga kazi. Toka hapo ndipo Diamond akaanza kuwa juu kwa umaarufu na kuwa kipenzi kwa watanzania.
Mapenzi na Mastaa Maarufu wa Bongo Movie na walembo kadhaa kumuongezea umaarufu na mashabiki
Wahenga walisema " Pesa ni sabuni ya Roho" wengine wakasema "Pesa ndo kila kitu" Mwanamziki yuhu Diamond mambo yalipoanza kumnyokea ndipo tulipoanza kusikia kuwa warembo kibao wanamnyemelea na wengine kumgombania kabisa.
Mwanzoni watu walimuwa wakimkejeli kuwa anasura mbaya; mara hooo ana mdomo mkubwa ( mrefu na mpana) na wengine kusema kila tusi walokuwa wakiliona linamfaa. Yote hayo yalisahaulika sasa kijana Diamond akaanza kushine; akaanza kutakata akapendeza mbaya. Nakumbuka kwenyevizuri kwenye video za nyimbo zake na shoo zake alikuwa akipenda kuvaa shuti na Necktie nyekundu.
Hapo sasa ndipo alipo mpata Mrembo Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na kuwa nae kimapenzi kisha kuishi wote. Ile kufanukiwa kudate na mrembo huyo miss tanzania mwaka 2006, Diamond alipaa kwa umaarufu na kujulikana sana nchini.
Hapo ndipo magazeti ya udaku na mengineo hapa nchini yalipoanza kuwandika front pages. Kila siku Diamond alikuwa akionekana page za mbele na story zake kuzidi kusambaa.
Pia kwa umri wake mdogo na kudate na Wema Sepetu aliyeonekana kumzidi umri nayo pia ilizidi kuwa habadi mjini na nchini na hapo ilikuwa miaka ya 2011 hivi.
Diamond alipata mashabiki wengi sana kwani mashabiki wote wa Wema Sepetu ilibidi wawe pia mashabiki zake kwani walimwita shemeji. Ikumbukwe kuwa Wema Sepetu alikuwa tayari maarufu kwa kipindi cha miaka kama 5 kwa hiyo alikuwa na mashabiki lukuki.
Kila siku iendayo kwa mungu1 Diamond alikuwa akiandikwa kwenye magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii akihusishwa na skendo na warembo kadha wa kadha.
Belle 9 yeye hakukuwa na skendo yoyote juu yake na warembo wa mjini.
Pia hakukaa kimya nae alizinduka na kuja na wimbo uitwae ' Nilipe Nisepe' wimbo ambao haulufanya vizuri kama zile nyingine za awali na ulizidi kufunikwa na upepo wa nyimbo za Diamond na umaarufu.
Baada ya wimbo huo wa Belle 9 ulofanya vibaya ; aliamua kukaa kimya kwa muda bila ya kutoa nyimbo huku mwenzie Diamond akizidi kufanya bandika bandua ya nyimbo tena zote zikiwa hit songs kama anavyofanya sasa hivi huyu bwana Mdogo Aslay!
Diamond alizidi kuachilia ngoma kali kama ' Lala salma; Mawazo; Nimpende Nani; Ukimwona; Nataka kulewa na Kesho. Nyimbo zote hizi zilikuwa mashine na zilizidi kupasua anga hapa nchini huku mahusiano yake na Mrembo huo Wema Sepetu yakizidi kunogesha mafanikio yake.
Mrembo huyo sasa kama mkewe alikuwa tena mwalimu wake wa tuition ya lugha ya kiingeleza. Unaambiwa Diamond alikuwa akila tuition ya kiingeleza kwani alikuwa hajui lugha hiyo.
Diamond ni mjanja aise! Alitumia vizuri huu msemo usemao " One Chance one Goal" alijua kuwa huko mbeleni Mungu akimsaidia atapata shoo za nje ya nchi
; atakuwa akisafiri kwenda majuu sasa akaona ajinoe kwanza lugha hiyo ngeni ili baadae asije pata taabu kwa.mawasiliano. Na nikweli alitoboa kwani Mrembo huyo inadaiwa alimpiga bonge la shule ba Diamond kuiva!
Ndo hapo sasa unaambia Diamond alipozidi kupata mashoo ya ukweli na ya mtonyo mnene ndani na nje ya nchi. Aliweza kupiga kolabo nyongi na wasanii kibao wa ndani na njee.
Hakuishia hapo; Nyota yake ilizidi kuwaka na kung'ara sana na alizidi kuwa na uwezo mzuri wa utungaji wa mashairi huku akiwakosha watanzania kwa sauti yake ya kipekee!
Aliachia nyimbo nyingi sana zilizotikisa hapa nchini na nje ya nchi pia kama:
“Mapenzi Basi”
“Uswazi take away remix”
“Nieleze”
“Natamani”
Kutoka kimapenzi na kumuoa Boss Lady Zari Mke Mganda; mke wa tajiri matata wa South Africa.
Diamond baada ya kuwa juu; mwaka 2013 alitoa wimbo wa Taifa uitwao Number One ambao ulitikisa nchi vya kutosha. Kumbe alipotoa ngoma hiyo alikuwa akimwimba mpenzi wake mpya Mganda The Boss Lady Zari.
Toka hapo mengi kuhusu zari the bossi Lady yakaanza kujulikana. Tukajua kuwa ni aliekuwa mke wa Kijana Tajiri matata Mganda aishie South.
Hapo sasa Diamond akazidi kuwa maarufu sana kwa kile kitendo cha yeye kuwa na uwezo kunyakuwa mke wa Billionnaire. Watanzania tukaaza kujiona fahari kuwa nasi tumo maana hayo tulikuwa tukiyasikia huko majuu kwa wasanii wamarekani!
Ikazidi kufamika kuwa Diamond basi nae ni Billionnaire wa kutupwa kwani angewezaje kula sahani moja na huyo Zari the Bissi Lady.
Diamond kuwa na zari basi alizidi kuwa maaruhi Afrika mashariki na kati na ulimwenguni kote. Diamond hakuwa tena mwenzetu!
Baada ya hiyo nyimbo ilofanya vizurikweli; Diamond alizidi kufanya vizuri kinziki ambapo baadae aliachilia nyimbo kama:
“Number One Remix” (featuring Davido)
“Mdogo mdogo”
“Bum Bum” (featuring Iyanya)
Lala Ukisinzia,Ntampata, Wapi,Nasema Nawe”,Nakupenda pia Nana.
Utanipendaga
Salome
Marry you
Hallelluya
Sikomi
Niache
N. k
MAFANIKIO YAKE . ( Diamond)
July; mwaka 2016 Jarida la Forbes la nchini marekani lilitoa wasanii matajiri zaidi duniani ,Africa na kanda mbali mbali ambapo kwa upande wa Africa mashariki.
Diamond platinum aliogoza kwa kuwa na utajiri wa dollar million 4.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua Nyumba yake ya south Africa.
Vitu vingine anavyomiliki ni Majumba ya kifahari Dar,Magari ya kifahari , Berber shop, Maduka ya nguo za mitindo ya kisasa na vingine Vingi.
Katika jarida hilo lilionyesha diamond akiwa anafanya wastani wa show 2 kwa wiki show 8 kwa mwezi na show 100 kwa mwaka ambapo show yake ya chini anakadiriwa kulipwa wastani wa dollar elfu 20,000 na show ya juu analipwa wastani wa dollar elfu 75,000
Mikataba yake na makampuni kama Cocacola,Vodacom na DSTV
Anamiliki lebel yake ya Wasafi Classic Baby! WBC. Ambayo kasign wasanii wengine wengi tu na lebel hiyo kuwa kivutio cha kila msanii ama chipukizi au mkongwe kupata nafasi ya kuingia ( kusajiliwa)
Jarida ilo linaonyesha pia diamond anaweza vaa vitu vyenye thamani ya dollar laki 150,000 ambazo ni zaidi ya milioni 350,000,000 za tanzania mwilini mwake kwenye shoo moja ambavyo ni Pete,cheni,viatu kofia,shati na suruali na vingine!
Nb: Kupitia Diamond; msanii nyota hapa nchini tunajifunza kuwa mafanikio huja kwa kujituma tu! Diamond ni msanii tajiri hapa Tanzania na kwa sasa ni Billionnaire. Hela zake si za kutia shaka kwani toka anaanza safari yake ya mziki tulikuwa tukiona mafanikio yake mpaka hapa alipo kwa sasa.
Mwanzo nimejaribu kuwaonesha jinsi gani alivyoanza masiaha ya kimziki pamoja na msanii mwenzie wote wakiwa ma underground nyota na baadae yeye kumzidi mwenzake mpaka hapa alipo!
Kila mtu akikazana na kupiga boot kwa kufanya kazi kwa kujtuma huku ukiwa na malengo hakika tutafanikiwa! >
No comments: