Rick Ross atia saini ili video yake na Diamond ichezwe kwenye TV Marekani
Wiki kadhaa zilizopita tulipokea taarifa kubwa za kolabo kati ya Mwimbaji Staa wa Bongofleva wa Tanzania Diamond Platnumz na Hiphop Star wa Marekani Rick Ross.
Leo December 1 2017 tumepokea updates kuhusu ngoma hiyo kwamba Rick Ross ametia saini ili kuruhusu ngoma hiyo ipigwe kwenye Radio na TV za Marekani kitu ambacho ni cha faida zaidi kwa Diamond Platnumz ambae anapata nafasi kwenye uwanja ambao hakuwahi kuupata.
Tayari ngoma hiyo imeanza kuonekana kwenye TV mbalimbali za kimataifa ikiwemo TRACE ambapo Diamond amemwagika humo ndani kwa Kiswahili na Kiingereza.
No comments: