'Selfie' yamponza mbunge wa CHADEMA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Urich Matei ameweka wazi sababu za kukamatwa kwa mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya CHADEMA, Peter Lijualikali, mara tu baada ya kuachiwa leo na polisi ambapo alikuwa rumande.
Kamanda Matei amesema sababu iliyopelekea mbunge huyo kukamatwa tena leo hii ni picha aliyopiga na kuposti mtandaoni huku ikimuonesha akiwa na Afisa mmoja wa Polisi
"Kuna picha alipiga na ofisa mmoja akaiweka mtandaoni, sasa unajua haya masuala ya mitandao unapoweka picha ya mtu, na mwenyewe amekiri kweli ni yake na yeye ndiye ameposti, sasa bado tupo naye kwa mahojiano zaidi", amesema Kamanda Matei.
Leo asubuhi mbunge huyo alikamatwa na polisi muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kuahirisha kesi inayomkabili.
No comments: