Sugu Awapiga Mkwara CCM

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amefunguka na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawawezi kulikomboa jimbo la Mbeya Mjini hata kwa mabavu kwani anasema watu wa Mbeya hawajaribiwI hata Kikwete na Magufuli wanatambua hilo.

Sugu amesema hayo alipokuwa akihojiwa na MCL na kudai kuwa amesikia CCM wanasema wanataka kukomboa jimbo la Mbeya Mjini na kudai kuwa hawataweza kwa kuwa hata wao CHADEMA hawajalala.

"Wananchi bado wanaridhika na sisi kwa hiyo njia pekee watakayofanya labda watumie mabavu na kwa kutumia mabavu CCM Mbeya wanajua, Kikwete anajua, Magufuli anajua kwamba kwa mabavu kwa Mbeya uwezo huo hawana kwa sababu watu wa Mbeya hawajaribiwi na hilo tunalithibitisha hata kwenye Kata ya Ibighi wameleta mchezo mchezo wao kote walikoleta kwenye kata 42 lakini walipofika Ibighi tuliwapiga 'Stop' tukawathibiti" alisema Sugu

Sugu aliendelea kusema kuwa "Kama kwenye uchaguzi mdogo wa Ibighi ambao kulikuwa na resources zote za mkoa ziliwepo pale na wakashindwa kutumia mabavu watawezaje kwenye uchaguzi mkuu ambao resources zinakuwa mbalimbali, majimbo yanakuwa saba huko kote hao polisi wa kuwapeleka hawana kama ambavyo waliweza kukusanya polisi wa mkoa mzima kuwapeleka kwenye Kata ya Ibighi na bado wakashindwa" alisisitiza Sugu
>

No comments: